MIKOPO NAFUU
YA HARAKA
Tumesaidia mamia ya wateja kuboresha maisha yao, kukuza biashara zao, na kusimamia fedha zao kwa njia ya maadili, uwazi na ujumuishi wa kifedha.
Kuhusu sisi
Bayalimo Microfinance ni taasisi ya kifedha iliyoanzishwa tarehe 16 Mei 2024.
Taasisi hii inajihusisha na utoaji wa huduma za kifedha kwa watu binafsi na taasisi mbalimbali
nchini Tanzania. Tunahudumia wajasiriamali wadogo na wakubwa, wafanyakazi wa serikali,
wafanyabiashara, pamoja na madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, kupitia mikopo nafuu na
rahisi inayolenga kuwawezesha kukuza biashara zao na kuboresha maisha yao.
Taasisi hii imeanzishwa kwa lengo la kuendeleza ujumuishi wa kifedha na kuhakikisha kila mtanzania
anapata fursa ya maendeleo. Tangu kuanzishwa kwetu tumesaidia mamia ya wateja kuboresha maisha yao,
kukuza biashara zao na kusimamia fedha zao kwa njia ya maadili, uwazi na ujumuishi wa kifedha.
Makao makuu yetu yapo jijini Mwanza, na tunajivunia kuwa karibu na
wateja wetu ili kuwahudumia kwa ufanisi na uwazi.
Dira Yetu
Kuwa taasisi inayoongoza katika sekta ya microfinance Tanzania.
Dhamira na Malengo Yetu
- Kusaidia wajasiriamali na wafanyabiashara kwa kuwapatia mikopo nafuu itakayochochea ukuaji wa kifedha kwa wote.
- Kutoa huduma bora, nafuu na zenye kumlenga mteja, kwa kushirikiana na sekta binafsi na ya umma, ili kuwawezesha watu binafsi na taasisi mbalimbali kufikia malengo yao ya kiuchumi na kukuza uchumi wa kila mmoja mmoja.
- Kuhudumia waendesha pikipiki (bodaboda) kupitia mikopo rahisi na nafuu, tukianzia na Umoja wa Waendesha Pikipiki Mkoa wa Mwanza (UWP), na kupanua huduma hadi kufikia waendesha pikipiki wote Tanzania nzima.
Misingi yetu
SEKTA TUNAZOLENGA
Sekta Tunazolenga
- Biashara Ndogo na za Kati (SMEs)
- Kilimo na Biashara ya Kilimo
- Wafanyakazi wa Umma
- Biashara za Rejareja
- Sekta ya Ujenzi na Ufundi
- Sekta Isiyo Rasmi
- Taasisi za Elimu
- Vituo vya Afya na Huduma za Matibabu
- Usafiri na Vyombo vya Usafiri
Wateja Wetu
- Wajasiriamali na Wafanyabiashara Wadogo
- Wafanyakazi wa Serikali na Taasisi Binafsi
- Vikundi vya Kijamii na Vyama vya Ushirika
- Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Shule
- Biashara Changa (Startups) na Zilizokua
- Madereva pikipiki (Boda boda)
Mikopo yetu
Uzoefu Wetu
Tukiwa na mtandao unaokua kwa kasi nchini Tanzania, Bayalimo Microfinance ina uzoefu mkubwa katika kutoa suluhisho endelevu za kifedha. Timu yetu ina utaalamu katika usimamizi wa fedha, tathmini ya mikopo, na huduma kwa wateja — jambo linalotuwezesha kuhudumia wateja wa aina mbalimbali kwa ufanisi.
Kwanini Utuchague?
- Huduma Zinazomjali Mteja: Tunazingatia mahitaji yako binafsi kwa masharti rafiki na usaidizi wa karibu.
- Upatikanaji Haraka wa Mikopo: Tunachakata mikopo kwa haraka ili kukidhi mahitaji ya dharura.
- Suluhisho Maalum: Mikopo inayobadilika kulingana na kipato na malengo ya mteja.
- Wateja Wanatuamini: Tuna rekodi nzuri na mahusiano thabiti katika sekta mbalimbali.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Pata majibu ya haraka kuhusu huduma na mikopo yetu Bayalimo Microfinance.
Ninawezaje kuomba mkopo Bayalimo Microfinance?
Unaweza kuomba mkopo kwa kutembelea ofisi yetu na kujaza fomu ya maombi. Tunahitaji nakala ya kitambulisho, taarifa ya kipato, na wadhamini kulingana na aina ya mkopo.
Ni aina gani za mikopo mnazotoa?
Tunatoa mikopo ya biashara, binafsi, ya vikundi, ya mishahara, mikopo ya dharura, mikopo kwa bodaboda pamoja na ushauri wa kifedha kwa wateja wetu.
Kwa muda gani ombi la mkopo huchakatwa?
Mikopo midogo na ya dharura huchakatwa ndani ya siku 1–2, huku mikopo mikubwa ya biashara au vikundi ikichukua siku 3–7 kulingana na ukaguzi wa nyaraka.
Ninawezaje kufungua akaunti ya mteja?
Fungua akaunti kwa kutembelea ofisi zetu na kuwasilisha kitambulisho halali na mawasiliano yako. Akaunti yako itakuwezesha kufuatilia marejesho na kupata taarifa za kifedha kwa urahisi.
Je, naweza kupata taarifa za mkopo wangu kwa simu?
Ndio, utapata ujumbe wa simu, pia unaweza kupiga simu kwa watoa huduma wetu ili kufahamu salio na ratiba ya marejesho.
Ni njia zipi za malipo mnazokubali?
Tunakubali malipo kupitia benki, Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money, na malipo ya moja kwa moja ofisini.
Nitajuaje tarehe ya kurejesha mkopo?
Ratiba ya malipo inatolewa wakati wa kusaini mkataba wa mkopo. Pia utapokea ujumbe wa kukumbushwa kabla ya tarehe ya marejesho.
Je, kuna adhabu kwa kuchelewa kulipa?
Ndio, ada ndogo ya ucheleweshaji hutumika ili kuhakikisha nidhamu ya kifedha, isipokuwa kwa hali maalum zilizoidhinishwa na menejimenti.
Our Staff Team
Mawasiliano Yetu
Wasiliana nasi
Ofisi yetu
Mwanza, Tanzania
info@bayalimomicrofinance.co.tz
Tupigie
+255 762 475 85
+255 741 875 859
Saa za kazi
Jumatatu - Ijumaa
Saa 2:00 Asubuhi – Saa 11:00 Jioni